Kiswahili

Mwanzisho wa „Audiowalk“

Habari! Sisi ni muhungano wa kundi la Decolonize Dortmund. Tulishughulika na jambo la ukoloni wa zamani wa mji wa Dortmund. Katika matembezi haya ya sauti utaongozwa kupitia stesheni mbalimbali katika eneo la mjini Dortmund, ambazo zinaonyesha ni kiasi gani historia ya ukoloni wa Ujerumani bado iko katika miundombinu ya sasa. Hatutaki tu kuonyesha picha ya ukoloni ambao haujachakatwa mji wa Dortmund, lakini pia kuiweka katika muktadha wa hali ya kisiasa na mahesabu ya wanasiasa wa Ujerumani, wafanyabiashara, wamishonari, n.k. Historia ya ukoloni wa Ujerumani ina madhara ambayo bado yanaweza kuhisiwa hadi leo, lakini historia hii haijadiliwi sana au hata kidogo na hata huwa inakataliwa. Sisi Kama mkusanyiko wa watu weusi na watu wa rangi, tunataka kuchangia katika kufanya maarifa kuhusu miunganisho na mitandao ya ukoloni ipatikane zaidi kwa watu weusi na watu walioathiriwa na ubaguzi wa rangi. Tunaamini ujuzi huu unaweza kutusaidia kupitia jamii hii. Zaidi ya yote, ni lengo muhimu kwetu kuonyesha unyanyasaji wa kikoloni ambao umefichwa katika miundombinu ya miji ya Ulaya. Miji ya Ulaya na hivyo pia miji ya Ujerumani huwa kama kuwakilisha na kukumbuka historia ya Ulaya vile, anaandika mtafiti wa mijini baada ya ukoloni  bwana Noa K. Ha (Ha:2021).

Hii ina maana ya kwamba historia ya nchi/bara inaonekana katika nafasi ya umma, yaani kwenye mitaa na viwanja, na watu muhimu kwa masimulizi haya ya kihistoria pia wanaheshimiwa kwa makaburi. Pamoja na hao, nafasi ya mijini pia ni mahali ambapo taifa na pia jiji hujitokeza kwa watu wa ndani na wageni. Kwa hivyo, kupitia jiji, kupitia mitaa, usanifu, miundombinu na minara/makaburi, hadithi inaweza kusimuliwa na itikadi zilizoathiri hadithi hiyo zinafaa huko. Miji ya Ulaya lazima iwekwe na kulainishwa katika historia ya michakato ya kikoloni na imperialism. Vile Ha (Ha:2021). Wao ni kwa ajili ya biashara, ushindi na mitandao ya unyonyaji. Kwa hiyo haishangazi kwamba uhusiano mwingi na historia ya ukoloni unaweza kupatikana. Hapa ndipo mkusanyiko wetu unapoingia. Tunataka kukumbuka kikamilifu vurugu za kikoloni ambazo zimejiweka katika anga za mijini, kama Noa K. Ha anavyoielezea. Hii ina maana ya kuionyesha hadithi hii, kuisimulia na hivyo kupunguza kuzaliana vurugu na unyanyasaji wa kikoloni.

Hadithi. ambazo hazijasimuliwa hazifai kusikilizwa tu, ni muhimu ili kuyatatua mambo na ukoloni wa zamani.Vituo ambavyo tumechagua vinatoe mchango mdogo katika hili Historia. Na sasa kwa vituo. Nenda kwenye eneo lililoonyeshwa kwenye ramani, anza faili ya sauti  (Audio data) na uache hadithi iingie. Vinginevyo, unaweza kujistarehesha nyumbani na kucheza faili za sauti. Ikiwa neno kutoka kwa maandishi halimaanishi chochote kwako, jisikie huru kulitafuta katika faharasa kwenye tovuti (website) yetu. Labda unaweza kulipata huko. Tafadhali kumbuka maonyo ya vichochezi kabla ya kusikiliza podikasti.Tunakutakia ziara ya mafunzo ya kuondosha ukoloni kupitia vituo vyetu!


Station 1: Robert-Koch Straße

tw: majaribio ya kibinadamu, ukatili wa kibaguzi

Ukitembea mashariki kando kando ya Kaiserstreet na maduka yake mengi, na restraunts na Cafe`s (mikahawa na mikahawa), utahipita ile Bismarck Café. ambayo inasimama kwenye kona ya Bismarckstreet. Barabara anayofuata, karibu mwisho wa Kaiserstrasse, utapata Robert-Koch-Strasse upande wa kulia. ambayo inakuongoza zaidi kwenye Makaburi ya Mashariki Mitaa na Barabara kote Ujerumani vinamkumbusha Robert Koch, Vile  inayomkumbuscha Robert-Koch-Strasse katika Kaiserviertel ya Dortmund.

Robert Koch alikuwa Daaktari wa Ujerumani ambaye mpaka waleo anachukuliwa kuwa maarufu kwa mtafiti aliyefanikiwa sana kwa Ujunguzi wa madawa wa karne ya 20.(most famous and successful medical reasearcher of the 20th century). Katika mwaka wa 1905 aliweza kupokea Tuzo la Nobel kwa uvumbuzi wa Pathojeni ya Kifua Kikuu.(Tuberkulosis erregers).Pia aliongoza Taasisi (Institute) ya magonjwa ya Kuambukizwa, Taasisi ya Robert Koch ya leo.  Kwa Dola (Kaiserreich) ya Ujerumani, ule ujuzi wa Madawa na utafiti wake ulitumika kuhalalisha Juhudi zao binafzi na matarajio yao ya Kikoloni. Hadi leo, uhalifu uliofanywa na Ujerumani wakati huo kwa jina la Sayansi umejadiliwa kidogo sana, ikiwa pamoja na jambo la kufanya Vipimo kwa Binadanu na Madawa ambayo hayajachunguzwa kupitia Vituo vya Sayansi wakati huo. Wanasayansi wa Ujerumani na wengineo kama Robert Koch walizitumia maeneo yaliokuwa chini ya Wakoloni. Maeneo katika Bara la Afrika na wenyeji wao kuwa kama Maabara ya majaribio,kufanya vipimo vya matibabu kwa wanainchi humo bila kikomo.

Mnamo 1906, Robert Koch aliongoza kile kinachoitwa safari ya Afrika Mashariki, Ambayo ni Tanzania na Uganda ya leo, kuchunguza magonjwa ya usingizi huko. Hii haikuwa safari yake ya kwanza ya kikoloni nje ya Uropa, Hapo awali alikua amesafiri kwenda nchini India kutafiti ugonjwa wa kipindupindu na kwenda New Guinea kupambana na malaria huko. Majaribio hatari yaliyofanywa kwa wanadamu hayakuwezekana nchini Ujerumani kwa sababu ya kuongezeka kwa malalamiko ya watu wengi humo nchini. Ziliwezekana tu kufanywa kwa zile inchi ziliyokua chini ya ukoloni hata bila Udhibiti ama kuluhuziwa .nao kulindwa na wanajeshi na polisi. Utafiti wa madawa kwa wanadamu huko alikikua jambo la kufanywa mara kwa mara katika makoloni hayo. Ugonjwa wa kulala huwa hunaenezwa na nzi wa tsetse na mwanzoni ulionekana katika Afrika Magharibi. Kupitia maendeleo ya wakoloni ya kufunganisha maeneo kwa ujenzi wa barabara ziliopitika, pamoja na reli ziliwawesheza kusafirisha malighafi (Rohsstoffe/Ressources) kwa njia za reli, waliweza kusisambasa zile nzi wa tsetse na huo Ugonjwa wa kulala pia. Kati kati ya mwaka 1901 na 1905 karibu robo moja milioni ya watu walikufa kutokana na huo ugonjwa wa kulala katika Afrika Mashariki.

Utafiti na upelelezi umeonyesha yakwamba ukoloni kutoka Ulaya ulichangia kiasi kubwa sana kwa kuyaenesha magonjwa ya mlipuko (Epidemie) bara la Afrika. Uganda, ambayo ilipakana na iliyokuwa Afrika Mashariki ya wajerumani, iliathirika sana na ugonjwa wa kulala, hata ingawa ilikuwa ni sehemu ya makoloni ya Waingereza na kulikuwa na ushindani mkubwa wa kibeberu katika bara hilo. Janga moto hilo lilionekana kuwa tatizo la sehemu zote na linapaswa kupigwa vita pamoja. lakini, msukumo huo wa kupigana kuhungamisha huo ugonchwa haukuwa kwa ajiri ya kibinadamu, ila kwa ajiri ya uthibitishi wa faida zao wenyewe. Kwa sababu ya hayo Magonjwa ya mlipuko kama magonjwa ya kulala, watu wengi sehemu kubwa walikufa ambao ndio walihitajiwa na wakoloni kua wafanyakazi.ili kuweza kufuata masilahi ya kiuchumi kama vile unyonyaji wa rasilimali za ndani.Wakoloni walinufaika na utafiti na matibabu ya magonjwa kama vile malaria. kwa sababu Afya yao Wazungu pia iliwawezesha kusongea ndani ya zile Nchi zaidi katika maeneo yao Wakoloni na hivyo kuhutuliza Utawala.

Robert Koch alikua anatumia Dawa inayoitwa Atoksili (Atoxyl), inayojulikana pia kama asidi ya Arsanilic, kutibu Ugonjwa wa kulala. Alikua anawapatia Wagonchwa hilo dawa haraka kwa dozi kubwa, badala ya kuongeza kiasi kidogo kidogo wakati wa hayo majaribio. Hii ilisababisha madhara makubwa kama vile kichefuchefu, kizunguzungu, maumivu ya kifafa, kupoteza uwezo wa kuona na hata kifo chanyewe. Ni wazi kutokana na maandishi ya Koch kwamba watu wagonjwa hawakutaka kuja kwa matibabu yake kwa hajiri ya kupenda kwao, ila walikua wanatafutwa na kulasimishwa kuletwa kwake. Wakati wa ukoloni, maneno haya yaliweza kumaanisha mambo mbalimbali, kutoka kwa majaribio ya kushawishi hadi vitisho vya adhabu hadi kulazimishwa kwa nguvu. Watu wengi walipinga, lakini upinzani wao ulivunjwa kwa nguvu na wakoloni. Misingi ya utafiti wa kimatibabu wa kikoloni ilikuwa na malengo ya kulingana na supra ubaguzi wa rangi ya ubora na kupitishwa kwa nguvu ya utawala. Kwa sababu ya kugonjeka zaidi na madhara mbaya, Kile kipimo cha juu ya dawa kiliondolewa na badala ya hapo awali na orodha ndefu ya dawa zingine zilizotumiwa,ambayo hapo awali ilijaribiwa kwa wanyama tu na ambayo baadhi yao haikujaribiwa kwa makusudi kwa wanainchi nchini Ujerumani. Lakini, wasiwasi kama hizo hazikuhesabika makusudi kwa nchi za makoloni. Ili kutokomesha nzi wa tsetse kama wasambaziaji wa ugonjwa wa kulala, Sehemu zote za ardhi zilisafishwa ili kuchukua nafasi yao ya kuishi – kwa imani ya kikoloni kwamba wanaweza kutawala asili.Lakini, mara nyingi walionekana tena katika sehemu zinine, ndiyo sababu watu walihamia kwingina na kupewa makazi mapya.Watu wengi walipoteza nyumba zao na riziki kwa sababu hiyo. Kati ya mwaka wa 1912 na 1914, Watu wa Duala ambayo sasa ni Kamerun walihamishwa kwa nguvu na kunyang’anywa ardhi yao, iliyohalalishwa na ripoti za matibabu ambazo zilihalalisha hii kama hatua ya kuzuia magonjwa.

“Mtu anaweza kuanza kuhamisha wakazi wote wa maeneo yaliyochafuliwa hadi maeneo yenye Afya; Watu walioambukizwa basi, kwa kuwa kiwango cha vifo kilikuwa kamili bila Matibabu, wataangamia bila ubaguzi, na tauni hiyo ingezima”.

Kauli hii ya Koch inaonyeza wazi kwamba yeye hakuwa na nia ya kuponya Ugonjwa huo kwa wakaaji wa Maeneo hayo. Mbinu nyingine ya udhibiti iliyotumiwa na Koch ilikuwa kutenga watu walioambukizwa kwa kuwafunga kwenye Kambi kama Jela. Kambi ya Koch,  Baadaye Kambi zingine za Wagonjwa wenye Ugonjwa  wakulala,  zilitumika kama Uwanja wa Majaribio ya Uafiti wa Matibabu kwa Wazungu.( European Madical Research), Koch aliendelea kuamini Atoxyl kuwa ndio dawa inayofaa zaidi, hata ingawa alijua kwa hiyo Dawa ilikua na Madhara, Katika kambi kumi na vituo sita vya Matibabu, ni wagonjwa 71 tu kati yao 3,033 walioponywa, na Watu 386 walikufa. Wagonjwa 1010 walifanikiwa kutoroka kutoka kwenye kambi hizo na hivyo kuepuka Majaribio hayo ya kutishia maisha.

Hiyo dhana ya makambi ilitumiwa baadaye Togo na Cameroon. Majaribio yalifanywa kwa miili ya Watu na Maandalizi zaidi ya Dazeni za Vipimo tofauti. Bila shaka, maslahi ya wale walioathirika hayakuzingatiwa.Walielezwa tu katika madokezo na shajara pekee kama vitu vya Utafiti na kwa hivyo wakaondolewa Utu kabisa.Kubagua na kupendelea watu ni Tabia ya dawa za Kikoloni.  Dawa na Bila shaka, mazoea ya Uponyaji yalikuwepo kabla ya kuwasili wa Wazungu. Kwa kuwa haya hayakulingana na mawazo ya Eurocentric, yalionekana kuwa hatari na kupigwa marufuku. Lakini madaktari wa kikoloni walikuwa wanategemea maarifa ya wenyeji na walitumia, kwa mfano, katika uwanja ile miti ya dawa au maelezo ya kuenea na dalili za magonjwa bila kuwatambua waanzilishi wa ujuzi huu. Baada ya utafiti (research) wa Koch, ilichukua miaka 20 kabla Kampuni ya Bayer iliweza kutengeneza dawa ya ufanisi inayoitwa Suramin kwa mafanikio. ya Huo Ugunduzi ulitumiwa kwa marekebisho ya kikoloni* na kutumiwa na propaganda za Nazis. Hata Ingawa majaribio yalifanywa kwa watu ambao walilazimishwa kukaa gerezani kwa maendeleo yake, bado mpaka waleo inachukuliwa kuwa mafanikio ya madawa ya kitropiki Ujerumani.

Kwa madawa ya kikoloni haikuwa ni malengo ya kusaidia watu, ila ilikuwa ni kupata maarifa mapya ya kisayansi ya Ujerumani na tasnia ya dawa (Pharma industry) na kufikia lengo la maendeleo ya uchumi kwa makoloni yao. Kwa hivyo, madaktari wa kikoloni waliwapa watu mafuta maumivu na kuwadunga maji ya chumvi au kuwatupa jangwani ili waweze kuona ni muda gani  wachukua kuishi huko.Lakini, hata wa leo kipindi cha ukoloni wa Wajerumani mara nyingi hupuuzwa kwa kusema kwamba Wajerumani walifanya utafiti tu, lakini jinsi vileutafiti ulivyofanywa haujadiliwi sana.

Tangu kutokea wa Corona, jina la Robert Koch, liko tena kwenye midomo ya kila mtu kwa ajili  yakupewa jina lake  ile Robert Koch Institute. RKI yenyewe hufanya uhalibifu huko wanadamu, ambayo Robert Koch na timu yake waliyotenda, kwenye ndani ya “Home page” yao kama „nyakati ya giza za kazi yake“, lakini bila kuishughulikia zaidi. Maandishi, ambayo yanatoa muhtasari wa kazi yake Robert Koch, hayaongei vyovyote ju ya hiyo kazi yake kwa nyakati za ukoloni. umuhimu ya waliotezeka kupitia vitendo vyake huwa unajukuliwa ati na ubora ya matokeo yake ya matibabu. Hii inaonyesha kinyama na mahofu ya ukoloni na kuhusika kwake Robert Koch ati kuonekana kua kama nia zake hazikwa mbaya.

Tangu miaka mingi, na mara kwa mara, mashirika ya kiraia yamekuwa yakitoa wito kwa Taasisi ya Robert Koch zile mitaa na Barabara ziliyopewa jina lake kubadilishwa jina. Taswira ya kikoloni-kibaguzi cha bara la Afrika kuonekana kama „eneo la magonjwa ya milipuko“ imabaki kujulikana hiyio mpaka waleo. Katika maripoti za vyombo vya habari kuhusu magomjwa ya ukimwi au malaria, bara la Afrika huwa linaelezewa kuonikana kuwa ni la nyuma, hatari na linahitaji msaada. huku wakipuuza uhusiano wa leo wa mamlaka ya kikoloni. Maendeleo na mafanikio ya kisayansi katika barani hayasemwi. Kwa msaada wa masimulizi haya, yanaonyesha vile Ulaya inaendelea kujionyesha kua kama mkombozi wa jamii zisizo za Ulaya. Mfano mzuri wa hivi majuzi ni ripoti ya ubaguzi wa rangi ya lahaja ya omicron* ya virusi vya corona, ambayo iligunduliwa nchini Afrika Kusini lakini imeonekana kuwa haikuanzia huko. Vile mambo mengine, kupitia kipindi cha “ZDF Today Journal” wanaonyesha picha za ubaguzi wa rangi na lile Rhine-Palatinate na “die welt” kuandika kutumia lugha ya kibaguzi. Pia Kauli ya madaktari wa Ufaransa, waliopendekeza kufanyiwa majaribio ya chanjo ya corona kwanza katika bara la Afrika, pia inaonyesha mwendelezo wa taswira ya bara la Afrika kama maabara ya uchunguzi.

Mwaka wa 2017, wazao wa Herero na Nama waliishtaki Ujerumani huko Merikani kwa mauaji yao yaliyofanywa na wanajeshi wa Ujerumani mnamo 1904-1908. Mashitaka hayo yanasema, pamoja na mambo mengine kuwa, madaktari wa Ujerumani waliwafanyia Wafungwa wa Herero walioishi majaribio ya kitibabu katika kambi za mateso. Hadi leo wanadai fidia kwa hili, lakini mahakama ya Marekani ilikatalia hicho kesi ya mauaji ya kijamii mwaka 2019. Kuanzia mwaka 1909 hadi 1913, mamia ya watu walikufa kupitia chanjo ya ndui ilipofanywa ambao isivyofaa.huko nchini Togo iliyokuwa koloni la Ujerumani. Wakati huo, chanjo ya ndui (small box) ilikuwa tayari imefanyiwa utafiti wa kutosha, lakini chanjo hiyo ilikuwa imeitishwa na muda wake iliposafirishwa kutoka Ujerumani hadi Togo, ndiyo maana madaktari wa kikoloni walianza kulitengeneza chanjo hiyo humu ndani ya nchi. Lakini, hawakufanya ujunguzi uliruhuziwa wa lazima wa ufanisi wa hilo chanjo.

Chanjo waliyotengeneza haikuwa na ufanisi. Kwa kuwa watu wakati huo hawakuwa na imani na madaktari wa kikoloni, Ila mamlaka ya kikoloni iliwalazimisha kuchanjwa. Hata leo, majaribio ya madawa bado yanafanyika katika nchi za Kiafrika ambazo hazikidhi viwango vya maadili. karibu nusu ya majaribio yote ya madawa yaliyofanywa katika nchi za Global South. Yanafanywa na Makampuni ya Marekani, kwa mfano, Kampuni ya madawa ya Pfizer, ambayo ilitengeneza chanjo ya Corona pamoja na BioNtech, ilifanya majaribio ya Dawa na Dawa isiyoiruhuziwa kwa Watoto Nchini Nigeria mnamo 1996, ambapo Watoto kumi na moja walikufa. Mwaka 2012 kulikuwa na Kampeni ya Chanjo ya Homa ya Uti wa mgongo huko Gouro, Chad, ikiungwa mkono na Wakfunzi wa Bill na Melinda Gates, ambapo Watoto 500 wenye umri wa Mwaka 1-15 walichanjwa. Baada ya muda mfupi, Watoto watatu waliugua na hali zao kuwa mbaya zaidi. Lakini, chanjo ziliendelea kwa siku zifuatazo. Watoto 105 waliugua, 40 kati yao wakiwa mahututi. Ahmat Hassan, Mwandishi wa Habari kutoka Chad, aliandika kuhusu kesi hii, ambayo haikuwahi kutatuliwa na ambayo haikuwa na mashitaka yoyote.

Alihisi kuwa Mnyororo wa baridi na chanjo hiyo ulikatika, na ukababisha visa vya ugonjwa huo. Pia anasema watoto hao hawakupata nafuu. Wakati wa mlipuko wa Ebola wa Mwaka 2014/15, watafiti, madaktari na Watu wa kujitolea walidondoka kwenda Sierra Leone.  katika kituo kikubua cha matibabu katika mji mkuu Freetown. Dawa ya moyo ya amiodarone ilitolewa na kutumiwa , ambayo, kulingana na utafiti wa maabara ya Ujerumani, pia ilifanya kazi nzuri ya kutibu Ebola, Kwa kuwa dawa hiyo haikuidhinishwa kama dawa ya Ebola na WHO na serikali ya Sierra Leone.

Kituo cha matibabu cha Lakka kilikuwa kinaendeshwa na Shirika lisilo la Kiserikali (NGO) la Italia „Emergency“.Wahudumu hao walikuwa wa kujitolea kutoka Uingereza.Majaribio hayo yaligundliwa na wao kwa sababu kule kudunga kwa kiwango kikubwa kulisababisha magonjwa ya kupumua na kuvimba kwa baadhi ya wagonjwa. Kiwango cha vifo kilikuwa 67%. Vipimo hivyio vilisimamishwa, lakini hakuna aliyehukumwa hapa pia. Hakukuwa na uchunguzi, kesi wala Fidia yoyote. Chernoh Bah alitafanya uchunguzi vile waliviofanya wazungu Utafiti na Madaktari kuhusu Ebola na kuandika kitabu kuhusu („Mlipuko wa Ebola katika Afrika Magharibi: Majambazi wa Biashara, Mashirika ya Kimataifa, na Wanasiasa Rogue“) ambamo pia analinganisha uhusiano na mwendelezo wa ukoloni bado nchini bara la Afrika. Hii ni mifano michache tu inayoonyesha mwendelezo wa ukoloni katika sera ya leo ya Kimataifa ya Afya